Swali: Kumepokelewa:

“Asiyejali mambo ya waislamu basi si katika wao.”

Ina maana kuwa mtu anatakiwa kufuatilia taarifa ya khabari kwenye vyombo vya khabari na kujua hali zao au ina maana nyingine?

Jibu: Mosi Hadiyth hii si Swahiyh. Wanachuoni wameizungumzia.

Pili kuyajali mambo ya waislamu hakukuwi namna hiyo. Kuyajali mambo ya waislamu ina maana ya kutatua matatizo. Matatizo yanatakiwa kutatuliwa. Haitoshi tu kuyatambua. Yule anayeweza kutatua matatizo ndio kuyajali mambo ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017