Swali: Wako wanaosema kuwa ile pesa inayohifadhiwa kwenye benki na baadaye benki inaizalisha na kuwalipa ribaa wateja wake ni aina fulani ya uwezekaji katika benki. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Si uwezekaji. Hukuweka pesa katika benki kwa ajili ya kuwekeza isipokuwa ni kwa ajili ya kuzilinda peke yake, kwa sababu unachelea zisije kuibiwa, kuchomeka na mfano wa hayo. Wewe unaweka pesa yako benki kwa ajili ya kuzilinda peke yake na si kwa lengo la kuzizalisha. Hata hivyo kama umeziweka kwa lengo la kuzizalisha inakuwa ribaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (30)
  • Imechapishwa: 18/02/2022