Kuweka Qur-aan ndani ya gari kama ulinzi

Swali: Inazingatiwa kuwa ni kutafuta ulinzi kwa maneno ya Allaah kuweka msahafu ndani ya gari ili uilinde gari dhidi ya shari?

Jibu: Hapana. Huku ni kuweka hirizi. Haijuzu. Msahafu hautumiwi kama hirizi. Msahafu unatumiwa kwa ajili ya kusoma na kudurusu. Haijuzu kuutumia kwa ajili ukuhifadhi wewe mwenyewe, gari yako au nyumba yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (35) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20-%208%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017