Kuweka nadhiri ya kufunga Rajab imechukizwa


Swali: Kuna mtu fulani aliweka nadhiri ya kufunga swawm kwa ajili ya Allaah (Ta´ala). Lakini hata hivyo ndani ya nafsi yake hakulenga kama afunga mwezi mzima kamili au afunge kwa kupumzika. Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya masuala haya? Je, inajuzu kwake kufunga mwezi mzima mfululizo au inafaa kwake kufunga kwa kupumzika?

Jibu: Ikiwa aliweka nadhiri tu kwa kuachia ya kwamba atafunga basi katika hali hiyo itakuwa inafaa kwake kufunga kwa kupumzika au kwa kufululiza. Ama ikiwa aliweka wazi kufululiza, akanuia au akalenga mwezi maalum, basi katika hali hiyo itamlazimu kufululiza. Isipokuwa ikiwa kama alilenga kufunga Rajab hapo itakuwa imechukizwa kuufunga. Badala yake atatakiwa kutoa kafara ya yamini.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=340&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 20/03/2018