Kuweka mkatikati bila kumuabudu – njia inayopelekea katika shirki

Swali: Ni ipi tofauti kati ya yule ambaye anamfanya mkati na kati kuwa ni sababu na yule ambaye anamchinjia, anamfanyia Rukuu´ au anamsujudia? Je, kuna tofauti kati ya hayo mawili?

Jibu: Ikiwa anamwabudu basi anakuwa kama huyo wa kwanza. Lakini akiwa hamuombi, hamchinjii na hamwekei nadhiri, lakini anadhani tu kuwa ni sababu inayomfikisha kwa Allaah, tunasema kuwa hii ni Bid´ah na njia inayopelekea katika shirki. Kwa sababu Allaah hakufanya kuwa ni sababu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 76
  • Imechapishwa: 30/08/2018