Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka baadhi ya majarida na magazeti maeneo ya taka? Ni ipi hukumu ya kula juu yake na kuyafanya kama meza ya chakula?

Jibu: Ikiwa unaona ndani yake kuna kitu katika majina ya Allaah, Aayah au Hadiyth basi unalazimika kuyanyanyua kwa ajili ya kuheshimu yaliyomo ndani yake au angalau kwa uchache ukate kile kipande kilichoandikwa Aayah, jina la Allaah au Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hakuna neno ukatumia muda wa kuwa hujaona ndani yake kitu kama hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 47
  • Imechapishwa: 04/06/2021