Swali: Ni jambo limekuwa lenye kuenea kati ya wanafunzi wanaoanza kuwafarikisha wanachuoni kwa kusema “Huyu ni Muhaddith na huyu ni Faqiyh”. Je, kuna tofauti kati ya hayo mawili? Ikiwa kuna tofauti ni yupi kati ya hao wawili ambaye ni mbora zaidi?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba wanachuoni wote wameibeba Shari´ah kwa njia moja wapo. Huyu ni Muhaddith, huyu ni Faqiyh, huyu ni mwanachuoni juu ya I´tiqaad, huyu ni mwanachuoni wa sarufi na mwengine ni mwanachuoni wa balagha. Hapana shaka juu ya hili. Mbora wa watu ni yule aliyekusanya kati ya Hadiyth na Fiqh. Lakini itambulike kuwa kuna Muhaddithuun ambao hawana Fiqh. Dalili ya hilo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Huenda yule mfikishaji akawa si mwenye kuelewa zaidi kuliko msikilizaji.”

Ni nani mfikishaji? Ni yule mwenye kunukuu Hadiyth. Mfikishaji ni yule aliyechukua Hadiyth kutoka kwa yule aliyeipokea, lakini Fiqh yake katika dini ya Allaah [ikawa na mapungufu]. Kwa hiyo si kila Muhaddith anakuwa Faqiyh kama ambavyo si kila Faqiyh anakuwa Muhaddith. Kwa mfano kuna wanachuoni wa Fiqh ambao wametilia umuhimu vitabu vya wanachuoni, wakavihakiki na kuvidhibiti. Lakini hata hivyo akawa ni dhaifu katika Hadiyth. Kuna wengine ni kinyume na hivo ambapo utawakuta wamezama katika elimu ya Hadiyth. Lakini hata hivyo ni mchache katika uelewa wa Hadiyth. Hatimaye utamuona anaonelea ujumla katika mambo ambayo si yenye kuenea, anaonelea umaalum katika mambo yasiyokuwa maalum n.k. Lakini tatizo si hili. Tatizo ni kule kuwagawa watu. Kwa msemo mwingine watu wakaonelea kuwa huyu ambaye ni Muhaddith haifai kumuuliza mambo yanayohusiana na Fiqh na huyu ambaye ni Faqiyh haifai kumuuliza mambo yanayohusiana na Hadityh. Hili ndio tatizo. Ni wajibu kuamini kheri na baraka kwa wanachuoni wetu. Baraka ninayokusudia ni ya elimu na tusiwazuie watu kutokamana na ile elimu walionayo. Kwa sababu ukizuia kutokamana na ile elimu inayopatikana kwa wanachuoni Shari´ah itachukuliwa kutoka kwa wepi? Ichukuliwe kutoka kwa wajinga? Hili ni kosa kubwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/864
  • Imechapishwa: 28/06/2018