Swali 184: Uwepo wa makafiri katika nchi hii kunahalalisha kuwaua na kuwavizia khaswa wale wanaojuzisha kitendo hicho wanatumia dalili kwa Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watoeni washirikina nje ya kiziwa cha kiarabu”?

Jibu: Kafiri akiingia kwa mkataba kutoka kwa mtawala au kwa amani au amekuja kutekeleza kitu muhimu kisha atarudi, basi haijuzu kumshambulia. Uislamu ni dini ya kutimiza na sio dini ya udanganyifu na khiyana. Kwa hiyo haijuzu kumshambulia kafiri ambaye yuko katika mkataba wetu na chini ya amani yetu. Haifai kwa msomi kusema kuwa Uislamu unawadanganya mayahudi na unawakhaini mayahudi. Haya hayatokamani na Uislamu. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Watoeni washirikina nje ya kiziwa cha kiarabu.”

ni Hadiyth Swahiyh[1]. Lakini haina maana ya kumuua ambaye kapewa mkataba na kapewa amani na wale walioko chini ya mikataba yetu. Bali jambo hilo linapatikana kwa mayahudi  na manaswara ambao hakuna baina yao na baina ya waislamu ahadi wala mikataba.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/63-makatazo-ya-kuwaacha-makafiri-wakamakinika-na-kutanua-katika-kisiwa-cha-kiarabu/ 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 373
  • Imechapishwa: 16/02/2020