Kuwavisha watoto mavazi yenye picha za viumbe wenye roho


Swali: Ni ipi hukumu ya kuwavisha watoto mavazi yaliyo na picha za viumbe wenye roho?

Jibu: Wanachuoni wanasema imeharamika kumvisha mtoto kile ambacho imeharamika kumvisha mkubwa. Kile kilicho na picha kumvisha mkubwa itakuwa ni haramu. Kadhalika kitu hicho kumvisha mtoto itakuwa ni haramu pia.

Kinachotakiwa kwa waislamu ni wao kususia mfano wa mavazi na viatu hivi ili watu wa shari na waharibifu wasituingilie kwa kutumia njia hii. Watapofanya hivo hawatokuwa na njia nyingine isipokuwa kuzileta katika nchi hii na kuzipuuzisha kati yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/275)
  • Imechapishwa: 04/06/2017