Swali: Kuna wanaovamia maimamu wa madhehebu manne na kupuuza juhudi zao kwa hoja hatutaki kufuata kiupofu. Twaomba ubainishe nafasi zao.

Jibu: Huyu nafasi yake yeye. Huyu ndiye aulizwe. Elimu yake imefikia wapi? Ni mjinga kiasi gani mpaka aongee namna hii? Huyu katoka kwenye medhehebu ya kisasa. Ni juu yake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na aheshimu wanazuoni na aheshimu vitabu walivyoandika. Asifugulie watu mlango wa kusengenya kwa elimu na kwa wanazuoni na vitabu vya Kishari´ah. Akawakimbiza kwavyo. Yaani ´amali zote za hawa Waislamu katika historia ni batili alipokuja mtu huyu? ´Amali zote za Waislamu na za maimamu ni batili? Ametakasika Allaah. Huyu twamuuliza elimu yake imefikia wapi? Huenda hata hana elimu yoyote. Anataka watu wawe kama Ahmad bin Habal, Maalik, Abu Haniyfah, Shaafi´iy, Awzaa´iy wanachukua katika Qur-aan na Sunnah moja kwa moja bila kurejelea vyanzo vya vitabu katika vitabu na misingi? Wamesema yakusema pia kuhusu al-Iraaqiy “al-Alfiyyah” na kitabu “ar-Rahbiyyah”. Huku ni kuiharibu elimu. Ni juu yake kutubu kwa Allaah na aandike makala nyingine ambapo atabainisha kosa kwa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/tg–1431-11-11.mp3 Tarahe: 1431-11-11/2010-10-18
  • Imechapishwa: 09/04/2022