Swali: Je, ni sahihi kwangu kuwauliza baadhi ya watu “Allaah Yuko wapi?” kisha niwabainishie baada ya hapo…

Jibu: Swali hili liliulizwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alimuuliza mjakazi wakati alipokuwa anampa mtihani. Alimuuliza:

“Allaah Yuko wapi?”

Akasema:

“Mbinguni.”

kwa kuashiria mbinguni.

Hivyo akasema “Mwache huru, hakika ni muumini”. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameuliza “Allaah Yuko wapi”.

Lakini Mu´attwilah kwao haijuzu kuuliza “Allaah Yuko wapi”, kamwe. Baadhi yao wanasema “Allaah Yuko wapi” maana yake ni “Allaah ni nani”. Ametakasika Allaah. Tangu lini “Yuko wapi” ikawa na maana ya “Ni nani”!!? Huu ni uongo juu ya lugha ya kiarabu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (47) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-04-08.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014