Kuwaua wadudu na wanyama wenye madhara nyumbani

Swali: Wadudu wanaokuweko nyumbani kama mfano wa sisimizi, mende na mfano wake – je, inafaa kuwaua kwa maji, kuwachoma au niwafanye kitu gani?

Jibu: Inafaa kuwaua wadudu hawa ikiwa wanaudhi. Lakini mtu asiwachome. Bali awaue kwa aina zingine za dawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanyama aina tano wote ni wachafu na wanauliwa katika Ihraam na nje ya Ihraam; nao ni kunguru, bundi, panya, nge na mbwa kichaa.”

Katika tamko lingine imekuja:

“… na nyoka.”

Hawa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza maudhi yao na kwamba ni wachafu. Kwa msemo mwingine wanaudhi na ameidhinisha kuwaua. Vivyo hivyo wadudu wengine mfano wake wanauliwa katika Ihraam na nje ya Ihraam wakileta maudhi. Mfano wa wadudu hao ni sisimizi, mende, mbu na wengineo wanaoudhi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/298) https://binbaz.org.sa/fatwas/1089/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%82%D8%AA%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%B4%D8%B1%D8%A7%D8%AA-%D9%85%D8%AB%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%86%D9%85%D9%84-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B5%D8%B1%D8%A7%D8%B5%D9%8A%D8%B1
  • Imechapishwa: 04/01/2020