Kuwatumia familia thamani ya kichinjwa wakati wa ´Iyd-u-Adhwhaa´

Swali: Sisi si watu tunaoishi hapa Saudi Arabia. Ni jambo lisilofichika kwako ya kwamba familia zetu wako katika haja kubwa ya kuchinja na kufaidika na nyama yake na ngozi yake na wengi wao ni mafukara. Je, inafaa kwetu kuwatumia thamani ya kichinjwa na kumuwakilisha mtu atakayekuwa naibu wetu pamoja na kujua ya kwamba malengo ni kudhihirisha nembo hii? Je, inajuzu kwetu kufanya hivo?

Jibu: Ikiwa mtu yuko katika mji fulani na familia yake iko katika mji mwengine, basi hakuna ubaya kwake akawakilisha mtu atakayechinja kwa familia yake badala yake ili familia yake waweze kufurahika kwa kichinjwa. Kwa sababu ikiwa atachinja katika mji wa kigeni hakuna yeyote atakayekula kichinjwa chake. Huenda asiwe anamjua yeyote anayeweza kumpa swadaqah. Kwa ajili hiyo tunaona kwamba yule aliye na familia basi awatumie familia yake kima ya kichinjwa na kuchinjwe huko.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (34) http://binothaimeen.net/content/746
  • Imechapishwa: 26/11/2017