Swali: Kuna walinganizi ambao hawaiti katika uasi dhidi ya watawala, lakini hata hivyo wanawasifu wale wanaofanya hivo na wanazungumza waziwazi juu ya makosa ya watawala na mawaziri. Ni ipi nasaha yako?

Jibu: Hapana shaka kwamba haya ni maneno maovu na kitendo hichi ni potofu. Tunamuomba Allaah amwongoze mtu huyu. Si kila mzungumzaji anatakiwa kufuatwa. Yule ambaye ameshikamana na Sunnah pekee ndiye anayetakiwa kufuatwa:

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah kwa yule mwenye kumtaraji Allaah na siku ya Mwisho na akamtaja Allaah kwa wingi.” (33:21)

Hili linahusiana katika mambo yote. Haitakiwi kumfuata mtu kwa sababu tu analo jambo zuri. Mtu akimsifu mwengine ambaye hakemei kutafuta baraka kwenye makaburi  wala kuyachinjia makaburi, basi hutakiwi kumjegea dhana nzuri.

Kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun; wao si ni wenye kuwajengea njia Shiy´ah? Mtu mwaminifu ambaye mimi namtambua vyema amenieleza namna ambavo kiongozi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun huko Syria alimwambia Haafidhw al-Asad kipindi cha siku zake tukufu:

”Hakuna yeyote ambaye amehukumu Dameski kama ulivofanya wewe.”

Hivi ndivo anavosema Ikhwaaniy kumwambia Nusayriy anayesema kuwa Allaah ni ´Aliy bin Abiy Twaalib. Hata wadurusi wanawakemea juu ya jambo hilo ingawa wote wanatokamana na madhehebu ya Baatwiyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Haqiyqat-ul-Bay´ah fiyl-Islaam wa Bayaan Shuruutwihaa wa Khatwar Naz´ihaa http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148858
  • Imechapishwa: 05/12/2020