Swali: Je, katika zama zetu hizi kuna Jarh na Ta´diyl kama ilivokuwa kwa wanachuoni wetu waliotangulia? Ni ipi hukumu kwa mwenye kusema kwamba leo hakuna Jarh na Ta´diyl, bali hili ni jambo ambalo limeisha kwa maimamu waliotangulia?
Jibu: Jarh na Ta´diyl ni katika elimu ya Hadiyth. Ama kuzungumza katika vikao na kuwatukana watu, huu ni usengenyaji na kueneza uvumi. Huku ni kujeruhi pasina kusifu. Haijuzu kufanya hivi.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-10-10.mp3
- Imechapishwa: 15/11/2014