Kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr watoto wanaoishi nchi nyingine


Swali: Mimi ni mmisri ninayeishi Amman. Nataka kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr watoto wangu wanaoishi Misri. Je, inajuzu?

Jibu: Ndio, ni lazima kwako kujitolea Zakaat-ul-Fitwr wewe na watoto wako ilihali uko Amman. Ni wako. Ni lazima kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr wao na mke wako hata kama wote wako Misri au sehemu nyingine. Ni wako. Ni lazima kwako kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr ile sehemu uliyoko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://binbaz.org.sa/mat/13882
  • Imechapishwa: 23/06/2017