Kuwatolea swadaqah maiti kwa wingi kwa mtazamo wa Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Kuna mtu amefariki na nyuma yake ameacha familia na ndugu ambao hupenda kumtolea swadaqah kama kichinjwa, kumtolea pesa, chakula, mavazi na vyenginevyo. Wananuia mambo yote haya kumwendea roho ya maiti huyo. Je, matendo haya yanamzidishia kheri matendo ya maiti yule? Je, swadaqah hizi ambazo nduguze wamemtolea zinamnufaisha maiti na zinamkurubisha mbele ya wema siku ya hesabu?

Jibu: Kumtolea swadaqah maiti kunamnufaisha. Ni mamoja iwe pesa au chakula. Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba kuna mtu alimuuliza akasema:

“Mama yangu amekufa na lau angelikuwa anatamka angelitoa swadaqah. Je, nimtolee swadaqah?” Akamjibu: “Ndio.”

Matendo mema yanamnufaisha maiti na pengine yakamfutia makosa yake.

Lakini inapaswa itambulike kwamba haitakiwi kukithirisha kuwatumia wafu matendo. Japokuwa ni jambo linalofaa katika dini lakini haitakiwi kukuthirisha, kama wanavofanya baadhi ya watu ambapo utawaona daima wanawatolea swadaqah wafu wao. Mtu anatakiwa kujitolea swadaqah mwenyewe na wengieno. Yeye mwenyewe anahitajia matendo mema. Kwa sababu siku moja atakufa kama alivyokufa mtu huyu. Kwa hiyo ni mwenye kuhitajia matendo kama anavyohitajia mtu huyu. Kutoa swadaqah daima sio katika matendo ya wema waliotangulia. Ama kufanya hivo baadhi ya nyakati ni sawa na ni jambo linalomnufaisha maiti. Mtu ana haki zaidi ya matendo yake kuliko mwengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anza na nafsi yako kisha wale walio chini yako.”

Ikiwa wema waliotangulia walikuwa ni wenye pupa zaidi juu ya matendo mema na juu ya kuwanufaisha maiti wao, hawakuwa wakifanya hivo sana. Hivyo inapaswa kwetu kuwaiga na tusifanye kitendo hicho kwa wingi. Lakini mtu akifanya hivo baadhi ya nayakati ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (06) http://binothaimeen.net/content/6692
  • Imechapishwa: 03/11/2020