Swali: Dada yangu anaishi katika mji wa ar-Riyaadh na nilikuwa nikimtembelea. Hivi sasa mume wake ameleta nyumbani dishi. Hivi sasa naona uzito kumtembelea; je, nimkate au nimkate na badala yake niwasiliane nae kwa simu tu? Pamoja na kujua ya kwamba pindi ninapoenda kumtembelea basi hulala kwao. Hivi sasa mimi naona haya kwa Allaah kulala kwake ilihali juu yangu kuna dishi chafu.

Jibu: Ni wajibu kwako kumuunga dada yako na kwenda nyumbani kwake. Unachotakiwa ni wewe kumnasihi mume wake kwa kiasi cha uwezo wako. Haijuzu kwa mtu kuwakata ndugu zake kwa sababu ya kwamba eti ni watenda madhambi. Amesema (Tabaarak wa Ta´ala):

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Tumemuusia mwanaadamu kwa wazazi wake wawili – mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu na kumwachisha ziwa katika miaka mwili – ya kwamba: unishukuru Mimi na wazazi wako; kwani Kwangu ndio pa kuishia. Lakini wakikung´ang´ania kuwa unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii na tangamana nao kwa wema duniani na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu. Halafu Kwangu ndio marejeo yenu na nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.” (31:14-15)

Swali linahusiana na hayahaya. Mtu yuko na wazazi wawili ambao wote wawili ni wenye kumshirikisha Allaah ambao wametumia juhudi kubwa kumfanya mtoto wao ashirikishe pamoja na wao.  Katika hali hii Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَلَا تُطِعْهُمَا

“… basi usiwatii.”

Lakini wakati huohuo amesema nini?

وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا

“… na tangamana nao kwa wema duniani… “

Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu kuwaunga ndugu zake, awalinganie kwa Allaah na awanasihi. Wakiitikia, basi hilo ndio lengo. Vinginevyo madhambi yako juu yao.

Atapowaendea na kuwaunga na wao wakamletea chakula na kinywaji basi ale na anywe maadamu mbele yake hakufanywi maasi kama kwa mfano wamefungua dishi hiyo na yeye huku akawa anaangalia mambo ya haramu. Katika hali hii basi anatakiwa kuwaambia wazime au aondoke zake. Wakikataa basi ni wajibu kwake kuondoka zake. Kwa sababu haijuzu kwao kushirikiana nao katika mambo ya maovu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (35) http://binothaimeen.net/content/775
  • Imechapishwa: 03/12/2017