Kuwaruhusu wasiokuwa Mahaarim kuingia alipo mke

Swali: Ni ipi hukumu mume kuwaruhusu kuingia watu ambao sio Mahaarim wa mke wake?

Jibu: Hapana neno ikiwa hakuna kukaa chemba. Hata hivyo haifai ikiwa ni kukaa chemba. Ikiwa mwanamke huyo anakaa chemba na mmoja wao haifai. Lakini ikiwa ni ndugu zake…

Swali: Katika kikao maalum?

Jibu: Hapana neno. Ajisitiri vizuri kisha aingie. Anaweza vilevile kukaa maoneo mengine. Nakusudia kwamba anaweza kuwaruhusu mabinamu zake, jamaa zake au wakwe zake. Haina neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21659/حكم-الاذن-بدخول-غير-المحارم-على-الزوجة
  • Imechapishwa: 10/09/2022