Kuwapunguzia bei baadhi ya wateja

Swali: Mimi ni mfanyabiashara na wakati mwingine najiwa na wateja ambapo nawapunguzia bei baadhi ya wateja na siwapunguzii wengine. Je, inafaa?

Jibu: Ikiwa hukuwadhulumu wengine kama mfano wa biashara ya sokoni, hakuna neno. Inafaa kuwapunguzia bei baadhi ya wateja na si lazima kuwapunguzia wote. Hakuna neno. Lakini haifai kuchukua bei ya ziada ya thamani inayouzwa masokoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (98) https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18006
  • Imechapishwa: 18/05/2019