Kuwapigia Kura Waislamu


Ama kuhusu wachaguzi, naonelea kuwa ni wajibu kuwapigia kura wale waislamu walioridhia wenyewe kutumbukia katika maangamivu haya. Hoja yangu ni kwa ajili ya kuzuia yale madhara makubwa kuliko yale madhara madogo. Kuwepo kwao katika mabunge kuna afadhali kuliko vyama vingine (kama vile wakomunisti, wafuasi wa Ba´th na wakanamungu) kuwepo huko. Kwa ajili hiyo nimewanasihi ndugu zetu kuwapigia kura wale wagombea ambao ni waislamu. Bila ya shaka mmesoma kuwa waislamu ndio wengi hivi sasa bungeni. Lakini hata hivyo naamini kuwa hawatoweza kubadili kitu bungeni. Kwa ajili hiyo naonelea kuwa mgombea ni kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mfano wa msomi ambaye haitendei kazi elimu yake ni kama mfano wa mshumaa; unajiunguza wenyewe na kuwaangazia wengine.”

Mgombea anajiunguza mwenyewe na pengine anajaribu kuwaangazia wengine kidogo. Hata hivyo matokeo yake mshumaa huu unateketea wote na kupoteza mwangaza wote. Hivi ndivyo ninavyoonelea katika swali hili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (31)
  • Imechapishwa: 28/01/2017