Kuwapiga wanafunzi kwa lengo la kuwafunza

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwapiga wanafunzi wa kike kwa lengo la kuwafunza na kuwahimiza watekeleze mambo ya wajibu yanayowapasa wazowee wasiyapuuze?

Jibu: Hapana neno kufanya hivo. Mwalimu wa kiume, mwalimu wa kike na mzazi wote wanatakiwa kuwachunga watoto na kuwatia adabu wale wanaostahiki kutiwa adabu wakizembea katika yale yanayowapasa ili wazowee tabia tukufu na ili wawe na msimamo katika yale yanayotakikana katika matendo mema. Kwa ajili hiyo imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waamrisheni watoto wenu kuswali wanapokuwa na miaka saba  na wapigeni kwayo wanapofikisha miaka kumi na pia watenganisheni katika malazi.”[1]

Mvulana anachapwa na vivyo hivyo msichana wanapofikisha miaka kumi na wakazembea katika jambo la swalah. Wanatakiwa kutiwa adabu mpaka wanyooke katika swalah. Inahusiana vilevile na mambo ya wajibu mengine katika masomo, kazi za nyumbani na mengineyo. Ni lazima kwa walezi wa vijana wa kiume na wa kike kuwatilia bidii ya kuwaelekeza na kuwatia adabu. Lakini kichapo kiwe kidogo kisichokuwa na khatari lakini kinachofanya kupatikana malengo.

[1] Abu Daawuud (495). Hadiyth ni Swahiyh. Tazama ”Naswb-ur-Raayah” (1/298) kwa tamko kama hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/506)
  • Imechapishwa: 27/06/2021