Kuwapiga vita wanafiki wanaofanya matendo ya shirki


Swali: Je, inawezekana mtu akapigana kwa silaha pamoja na wanafiki ambao hawaswali wala kufunga na wanafanya baadhi ya matendo ya Shirki na kufuru na wanajiita “Waislamu”?

Jibu: Watu hawa ni lazima wasimamishiwe hoja katika mahakama ya Kishari´ah na wathibitishiwe. Ni lazima kupatikane hili. Hakuna yeyote anayehukumiwa kuritadi isipokuwa mahakamani kwa Qaadhiy. Hilo litafanywa kwa dalili na uthibitisho. Sio masuala ya mwenye kutaka tu kumfanyia mwenzie Takfiyr anamfanyia Takfiyr. Hapana. Masuala haya yana dhwawaabit.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-13.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014