Kuwapeleka watoto katika mizunguko ya kielimu na vituo vya kuhifadhi Qur-aan wakati wa likizo


Swali: Ni zipi nasaha zako kwa wazazi juu ya watoto wao kuwa likizo kuhusiana na mizunguko kielimu ya pamoja na vituo vya majira ya joto?

Jibu: Nawanasihi wazazi wamche Allaah (´Azza wa Jall) juu ya yale majukumu ya watoto wa kiume na wa kike ambayo Allaah amewabebesha. Wanatakiwa kuwachunga sana na watazame ni wapi waendapi na ni wapi watokapo. Hakika wazazi wataulizwa juu yao siku ya Qiyaamah.

Kuhusu vituo vya majira ya joto na mizunguko ya kuhifadhi Qur-aan, basi mimi nawashauri wasimamizi wawapeleke watoto wao huko ili kule kuwa na faragha kusije kuwaangamiza kinafsi, kifikira na kimwili. Huenda faragha hii ikawapelekea katika mambo ambayo matokeo yake hayatakuwa mazuri.

Kwa hivyo nasaha zangu kwa wasimamizi wawapeleke watoto wao katika vituo vya kuhifadhisha Qur-aan au katika vituo vya majira ya joto.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/810
  • Imechapishwa: 25/03/2018