Swali: Inajuzu kumpa zakaah ndugu fakiri ambaye mshahara wake uko chini ya mshahara wangu?

Jibu: Ikiwa ndugu huyu fakiri mshahara wake haumtoshelezi juu ya familia yake, basi hakuna neno kumpa zakaah yako. Bali kuwapa zakaah ndugu ambao wanastahiki ambao mtu hawajibiki kuwahudumia ndio bora kuliko kuwapa watu wa mbali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swadaqah yako kuwapa ndugu inahesabika ni swadaqah na kuunga udugu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1020
  • Imechapishwa: 21/02/2019