Kuwapa watoto zawadi siku za idi


Swali: Ni ipi hukumu ya kuwapa zawadi watoto siku ya Idi kwa kuwa tumesikia baadhi ya watu wanasema kitendo hichi ni haramu kwa kuwa ni kujifananisha na makafiri?

Jibu: Hapana, sio haramu katika siku za Idi. Ni siku za furaha. Watoto wana haja ya ambaye atawafurahisha. Hakuna neno – in shaa Allaah.

Wamesema hili katika siku za ´Aashuuraa. Wamesema kuwa haijuzu kuifanya kuwa ni Idi na siku ya furaha. Hili halina asli.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-10-10.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014