Swali: Ni ipi hukumu ya kuwapa makafiri pesa au zawadi kwa ajili ya kuwavutia katika Uislamu?

Jibu: Hakuna neno kuwapa zawadi na pesa au kuishi naye katika nyumba moja kwa ajili ya kumvuta katika Uislamu. Lakini inapaswa kuzingatiwa uvutiaji ni lazima uwe muhimu kwa njia ya kwamba yule anayevutwa ni miongoni mwa watu ambao kuna matarajio juu ya wao kusilimu. Ama wakiwa ni miongoni mwa wale vigogo wa ukafiri ambao hakuna matarajio juu ya kusilimu kwao basi hawapewi kitu isipokuwa kama wanapewa kwa ajili ya kuzuia madhara yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/372)
  • Imechapishwa: 07/05/2021