Swali: Kuna baadhi ya watu ambao wanawalishiza wanyama wao juu ya makaburi kutokana na wingi wa majani yanayopatikana juu yake.

Jibu: Haijuzu kufanya hivi. Wanyama wasiingizwe kwenye makaburi kwa ajili ya kuwalishiza juu yake. Wakatie majani wewe na uwapelekee nje ya makaburi wale.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-11-6.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014