Kuwalingania Watu Sehemu Za Vijiweni


Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema “Ni lazima kwa mlinganizi (Daa´iy) kuwalingania walio masokoni…?” Anaendelea kusema “… kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivofanya kwenye soko la ´Uqaadhw”?

Jibu: Ndio. Mlinganizi anatakiwa kuwalingania watu kila mahali, Misikitini, masomoni na kadhalika. Kila sehemu ambapo watu watakusanyika awalinganie, awape mawaidha na awakumbushe. Kwa kuwa kule kukusanyika kwa watu ni fursa kwa mlinganizi. Badala ya kulingania mmoja mmoja, awalinganie wakiwa wote kwa pamoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (45) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014