Kuwalea na kuwazoweza wasichana malezi na adabu za Kiislamu

Swali 1051: Ni ipi hukumu ya wasichana ambao hawajabaleghe? Inafaa kwao kutoka nje pasi na kuwa na sitara? Inafaa kwao kuswali bila mtandio?

Jibu: Ni lazima kwa walezi wao kuwalea malezi ya Kiislamu. Kwa hivyo awaamrishe wasitoke isipokuwa wakiwa ni wenye kujisitiri vile viungo visivyotakiwa kuonekana kwa kuchelea fitina. Mlezi wao anapaswa kuwazoeza tabia njema ili isiwe sababu ya kuenea ufisadi. Vilevile amwamrisha kuswali kwa mtandio. Iwapo ataswali pasi na mtandio basi swalah yake inasihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah ya mwenye hedhi isipokuwa akiwa na mtandio.”

Ameipokea at-Tirmidhiy, Ahmad, Abu Daawuud na Ibn Maajah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 437
  • Imechapishwa: 08/09/2019