Kuwakuta watu wanaswali mkusanyiko baada ya kumaliza kuswali

Swali: Baadhi ya watu wanakuja katika muhadhara na muheshimiwa Shaykh unaswali ambapo baadhi yao wanakaa nje, wengine wanaswali Tahiyyat-ul-Masjid na wengine wanakaa chini. Ni ipi hukumu?

Jibu: Mtu akija katika mkusanyiko anatakiwa kujiunga nao. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka katika swalah ya Fajr katika msikiti wa al-Khayf katika ule mwaka wa kuaga. Akawaona watu wawili ambao hawaswali ambapo akawauliza juu ya hilo na wakajibu kuwa wameswali majumbani mwao. Akasema:

“Mkiswali majumbani mwenu kisha mkaja msikitini na mkakuta wanaswali mkusanyiko, basi mswali pamoja nao. Hakika kwenu itakuwa ni Naafilah.”

Kwa hiyo ukiingia msikitini na ukawakuta wanaswali wewe swali pamoja nao. Hata kama itakuwa ni Maghrib swali pamoja nao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1716
  • Imechapishwa: 21/04/2020