Kuwakodishia nyumba familia za makafiri

Swali: Anauliza kuhusu kuwakodishia nyumba familia ya makafiri au mashirika yanayowapa makazi makafiri?

Jibu: Inatakiwa kutahadhari kutokamana na jambo hilo. Kwa sababu kisiwa hichi sio kwa ajili ya makafiri. Bali haijuzu kuwaacha ndani yake wala watu wakachukuliwa wepesi jambo hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth ambayo ni Swahiyh:

“Kusikusanyike katika kisiwa hichi dini mbili.”

Vilevile aliacha anausia kabla ya kufa kwake kuwaondosha mayahudi na wakristo katika kisiwa hichi. Ni kisiwa ambacho ndio chimbuko la Uislamu, sehemu ya kuenezwa Uislamu na sehemu ya kudhihiri kwake. Kwa hiyo haitakikani wakakubaliwa makafiri kubaki ndani yake isipokuwa kwa sifa ya kuzuka au kwa haja yenye kuzuka kama mfano wa mjumbe, daktari mwenye kuitwa wakati wa haja kupitia kwa mtawala. Vinginevyo watu wamechukulia wepesi wafanyakazi hawa makafiri na wengine, jambo ambalo lina khatari na shari kubwa. Kwa hiyo ni lazima kutahadhari kutokamana na jambo hili na mtu awe mbali kutokamana na mambo yanayowavuta maadui wa Allaah katika kisiwa hichi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3626/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D8%A7%D8%AC%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D9%8A%D9%88%D8%AA-%D9%84%D9%84%D9%83%D9%81%D8%A7%D8%B1
  • Imechapishwa: 08/03/2020