Kuwakilisha shirika au mtu akuchinjie ´Aqiyqah

Swali: Kuna shirika ambalo linachukua mali na kuchinja [´Aqiyqah] badala ya kujifanyia mwenyewe. Je, naweza kuwawakilisha wao wanifanyie hilo?

Jibu: Ndio. Wanachuoni wamefutu kujuzu kwa hilo. Kumpa wakili pesa akakununulia na kukuchinjia kisha ikagawanywa na hili litakuwa linatosheleza kwako. Lakini bora zaidi kuliko hili ni wewe mwenyewe kujinunulia na kujichinjia mwenyewe.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Ikhlaasw-ud-Diyn lillaah”
  • Imechapishwa: 06/10/2020