Kuwakilisha mtu amuhijie ambaye ni muweza kimwili na kimali

Swali: Mtu akinuia kujifanyia hajj mwaka huu. Kisha baadaye baba yake akajua kuwa anataka kufanya hajj akasema kuwa hiyo ni hajj yake. Je, inafaa kwangu kubadilisha nia hii wakati bado niko katika nchi yangu pamoja na kujua ya kwamba mimi na baba yangu tayari tumeshafanya ile hajj ya kwanza ambayo ndio nguzo?

Jibu: Ikiwa baba huyo ambaye ameomba hajj hiyo badala yake afanyiwe yeye ni muweza wa kuhiji, basi hili halimfai kitu. Kwa sababu maoni yenye nguvu ni kwamba yule mwenye uwezo wa kujifanyia hajj ima afanye mwenyewe. Ama kusema awakilishe mtu haimnufaishi kitu. Haijalishi kitu hata kama ni hajj iliyopendekezwa tu. Tunasema akiwa ni muweza basi ajifanyie mwenyewe. Akiwa si muweza basi hakuna kinachomlazimu na wala usimwamrishe nayo yeyote.

Tunasema kama yuko na mali basi ateue mtu akafanye ile hajj ya faradhi. Utapewa ujira na thawabu. Hilo ni bora kuliko wewe kwenda katika hajj ambayo ni sunnah. Utakuwa umemsaidia kutekeleza jambo la wajibu. Tusemeje juu ya yule anayemwambia mtoto wake amuhijie? Si sahihi. Haikupokelewa mtu akamuhijia mwingine isipokuwa ile hajj ya kwanza ya faradhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1189
  • Imechapishwa: 14/07/2019