Swali: Je, ni lazima kwangu kuwaamrisha swalah wale wanaofanya biashara baada ya adhaana ya kwanza siku ya ijumaa ambapo nikawakataza biashara wanayofanya?

Jibu: Ni lazima kwako kuamrisha mema na kukataza maovu baada ya adhaana ya pili ya ijumaa. Lakini Khatwiyb akianza kukhutubu basi ni lazima kwako kusitisha. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utakapomwambia mwenzako siku ya ijumaa “nyamaza” na huku imamu anatoa Khutbah umefanya upuuzi.”

Maneno yako “nyamza” kumwambia ni kuamrisha mema na kukataza maovu. Pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Umefanya upuuzi.”

Hii ni adhabu. Hizi sio thawabu ni adhabu.

Muulizaji: Wanafanya hivo katika adhaana ya kwanza?

Jibu: Katika adhaana ya kwanza una haki ya kuwakataza mpaka pale Khatwiyb atakapoanza kutoa Khutbah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1549
  • Imechapishwa: 19/04/2019