Swali: Kipindi cha mwisho kumedhihiri baadhi ya wazazi ambao wanawanyoa watoto wao wadogo nywele zao kwa mitindo yenye kutoka nje au mitindo ya kigeni kama ya kizungu na mingineyo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hukumu ya hilo imebainishwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Kwa hiyo mtu akikata nywele za watoto wake – ni mamoja wa kiume au wa kike – kwa mitindo ya vichwa vya makafiri, basi mtu huyo ni mwenye kupata madhambi. Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) amesema hali ya kuwa ni mwenye kuwekea taaliki Hadiyth hii inayosema:

 “Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

“Hadiyth hii hali yake ya chini kabisa ni uharamu ijapokuwa udhahiri wake unapelekea ukafiri kwa yule mwenye kujifananisha nao.”

Kwa sababu amesema:

“Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Kwa hiyo ni lazima kwa mtu kumcha Allaah Mola wake. Mtu atambue kuwa ataulizwa juu ya namna anavyowalea watoto wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1066
  • Imechapishwa: 14/03/2019