Swali: Ni ipi hukumu ya kukata nywele za wasichana kama wafanyavyo wanawake wa kifaransa? Ni lini unaanza umri wa uharamu? Kuna ambao wanasema juu ya mtoto wa kike ambaye ana miaka miwili au mitatu kwamba bado ni mdogo.

Jibu: Mwanawake kukata nywele zake ni jambo wanachuoni wametofautiana:

1 – Kuna wanaosema kwamba ni haramu.

2 – Kuna wengine wanasema kwamba imechukizwa.

3 – Wapo wengine wanasema kwamba inafaa.

Lakini ikiwa kukata nywele huku ni kwa njia ya kujifananisha na wafaransa au makafiri wengine ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu chake “Iqtidhwaa´-us-Swiraat al-Mustaqiym”:

“Hali ndogo iwezayo kusemwa juu ya Hadiyth hii ni uharamu japokuwa udhahiri wake unapelekea ukafiri kujifananisha na wao.”

Wanawake wengi wanasema kuwa malengo yao sio kujifananisha. Wanajibiwa kwa kuambiwa kukipatikana kujifananisha basi hakuangaliwi malengo. Kujifananisha ni ule muonekano. Kukipatikana muonekano ambao unafanana na ule wa makafiri, basi kujifananisha kumeshatokea. Ni mamoja wewe uwe umekusudia hivo au uwe hukukusudia. Hii sio ´ibaadah. Haya ni mapambo. Ikiwa mapambo haya tayari yanafanywa na makafiri basi haijuzu kwa mtu kujipamba nayo.

Kujengea juu ya hili tunasema kuwa haijuzu kwa mwanamke kuzikata nywele zake kama wakatavyo vichwa vya wanawake wa kifaransa au wengineo katika wanawake wa kikafiri.

Kuhusu ukataji mdogo kwa ajili ya kumpambia mume – kwa sharti isiwe kukata sana kiasi cha kwamba kunapelekea kufanana na vichwa vya wanaume – natarajia kuwa hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/813
  • Imechapishwa: 17/02/2018