Kuwaita watu wanaoshikamana na mafunzo ya dini kwamba wana msimamo mkali


Swali: Mara nyingi tunawasikia waislamu wasiokuwa na elimu wakiwaita wale waislamu wanaoshikamana na dini ya kwamba ni wenye msimamo mkali. Ni kipi kidhibiti cha kuwa na msimamo mkali?

Jibu: Yule mwenye kuitendea kazi Qur-aan na Sunnah sio kuwa na msimamo mkali. Kuna watu ambao wanawachukia watu wa kheri na kuwaambia kuwa ni wenye msimamo mkali na wenye wasiwasi. Mtu akiwa amenyooka katika kumtii Allaah na ni mwenye kuheshimu faradhi za Allaah halafu akawepo mtu mwenye kumfanyia mzaha kwa ajili ya hayo ni kama vile makafiri walivyokuwa mzaha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakimwambia kwamba ni mwendawazimu, mchawi na kuhani.

Ama ikiwa kweli mtu ana ususuwavu katika ´ibaadah kwa njia ya kwamba anazidisha juu yake na anaifanyia ugumu nafsi yake, huyu ni kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna yeyote atayeifanyia dini ugumu isipokuwa itamshinda.”

Yule ambaye anavuka mpaka uliyowekwa katika Shari´ah ndiye ambaye anatakiwa kuambiwa kuwa amekhalifu yaliyowekwa katika Shari´ah. Ama akiwa ni mwenye kunyooka kwa njia ya kwamba anatekeleza yale Allaah aliyomuwajibishia na kujiepusha, yale Allaah aliyomuharamishia na anaichunga nafsi yake kutokamana na maasi si sawa kwa mtu kumtuhumu kwa tuhuma hizo. Kumtuhumu kwa hayo ni maasi na ni kujifananisha na makafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 03/01/2018