Kuwaita Mitume na waja wema wakati wa shida na khofu

Swali: Baadhi ya watu wakati wanapopatwa na kitu au wakaogofywa na kitu wanaita na kusema:

“Enyi Mitume! Enyi watu wema.”

Ni ipi hukumu ya kusema hivo?

Jibu: Ulinzi unaombwa kutoka kwa Allaah. Huku ni kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Haya ni maombi. Du´aa ndio aina kubwa ya ´ibaadah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Du´aa ndio ´ibaadah.”

Bi maana ndio aina kubwa ya ´ibaadah. Haijuzu kumuomba asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 07/07/2018