Swali: Kipindi cha mwisho masomo ya kigeni ni jambo limeenea kwa kupitiliza katika nchi yetu kiasi cha kwamba imesemekana kwamba kuna masomo zaidi ya mia moja ambapo ar-Riyaadh kuna masomo thelathini, mashariki kuna masomo ishirini na nne, Jeddah kuna masomo ishirini na tatu, al-Qaswiym kuna masomo moja na namna hii yameenea katika mikoa. Ni ipi hukumu ya kuwaingiza watoto wetu katika masomo haya? Ni ipi humu ya kukodisha majumba juu ya lengo hili?

Jibu: Kitu cha kwanza kunatakiwa kutazamwe mifumo yake iko vipi na ni yepi yanayokhofiwa katika mustakabali? Kwa sababu mwaka wa kwanza mfumo wake unaweza kuwa wenye kusalimika asilimia kwa mia. Lakini mwaka wa pili ukabadilika na matokeo yake mtu akawa ameingia katika kushiriki na kwenye mtego wake asiyoweza kutoka.

Pili: Naona kuwa haifai kuwaingiza watoto wetu katika masomo haya kabisa. Kwa sababu vovyote yatavyokuwa masomo yetu ni bora kuliko hayo na himdi zote anastahiki Allaah. Masomo yaliyo chini ya wizara ya elimu yanakidhi kiu na yanatosha. Maoni yangu ni kwamba haifai kwa yeyote katika sisi kuwaingiza watoto wake wa kiume au watoto wa kike katika masomo haya. Ni lazima kuyasusa. Haya ndio maoni yangu juu ya masomo haya. Kuhusu uwekwaji wa masomo haya jambo hili halinuhusu mimi wala nyinyi. Yanawahusu watu wengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69) http://binothaimeen.net/content/1554
  • Imechapishwa: 24/02/2020