Swali: Mimi ni mwalimu wa mada ya Qur-aan tukufu. Lakini naona baadhi ya wanafunzi wanasoma Qur-aan pasi na wudhuu´. Je, inafaa kwao kugusa msahafu?

Jibu: Watoto wadogo ambao hawajafikia uwezo wa kupambanua ni sawa wakasoma Qur-aan pasi na twahara. Lakini wasiachwe wakagusa msahafu. Waandikiwe Aayah kwenye ubao na mfano wake uandishi wa muda fulani kwa kiwango cha haja. Salaf walikuwa na desturi ya kuwafunza watoto Qur-aan na wanawaacha waguse vibao vilivyoandikwa Qur-aan kwa ajili ya kuwafunza. Kuhusu ambaye ameshakuwa na uwezo wa kupambanua mambo anatakiwa kuamrishwa kutawadha kwa ajili ya kugusa msahafu kabla ya kuingia kwenye somo la Qur-aan. Kwa sababu huyu twahara na ´ibaadah nyenginezo zinasihi kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 48
  • Imechapishwa: 05/06/2021