Kuwafanyia tohara watoto wa kike


Swali: Baadhi ya nchi za Kiislamu zinawafanyia tohara watoto wa kike hali ya kuamini kwamba kitendo hicho ni faradhi au kilichopendekezwa.

Jibu: Kufanyia tohara wasichana ni jambo lililopendekezwa kama vile kuwafanyia tohara wavulana pale atapopatikana anayejua vizuri jambo hilo katika madaktari wa kiume au wa kike. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mambo ya kimaumbile ni matano; kutahiri, kutoa nywele za sehemu ya siri, kupunguza masharubu, kukata kucha na kunyofoa nywele za kwapani.”

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/46)
  • Imechapishwa: 06/08/2021