Kuwafanyia Tabdiy´ Maswahabah Kwa Kusema Adhaana Ya Kwanza Ijumaa Ni Bid´ah


Swali: Je, adhaana ya kwanza siku ya Ijumaa ni Bid´ah na ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema hivo?
Jibu: Kwa hivyo Makhaliyfah waongofu watakuwa ni watu wa Bid´ah. Kwa kuwa adhaana ilikuwepo katika zama za Khaliyfah wa tatu ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh), Muhaajiruun na Answaar. Kwa mujibu wa madai ya mjinga huyu[1] ina maana watakuwa watu wa Bid´ah.
[1] Tazama http://firqatunnajia.com/katika-masuala-haya-al-hajuuriy-ni-mjinga/
  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-5-29.mp3
  • Imechapishwa: 18/01/2017