Kuwafanyia mzaha wanachuoni ni sawa na kumfanyia mzaha Mtume?

Swali: Je, anayewafanyia istihzai wanachuoni analingana na anayemfanyia istihzai Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inapokuja katika hukumu?

Jibu: Kumfanyia istihzai Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni khatari zaidi. Kuwafanyia istihzai wanachuoni vilevile ni jambo baya kwa sababu ndio warithi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanachuoni ndio warithi wa Mitume.”

Mwenye kufanya mzaha na wanachuoni amewafanyia mzaha warithi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Hivyo atakuwa amewafanyia ishtihzai Mitume kwa njia ya ulazima. Kwa nini anawafanyia istihzai? Si kwa jengine ila ni kwa sababu ya ile elimu waliyorithi na waliyobeba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 141
  • Imechapishwa: 23/12/2018