Kuwafanyia istihzai watu wa dini

Swali: Wapo ambao wanafanya istihzai na watu walioshikamana na dini na wanasema kwamba ni wasusuwavu. Je, kunachelewa juu yao kwamba kitendo hichi kikafasirika ni kumfanyia istihzai Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hapa kunahitajia upambanuzi; akiwachezea shere kwa sababu ya dini yao basi kitendo hichi ni kufuru na kuritadi. Ama akiwafanyia istihzai wao kam wao na si kwa sababu ya dini yao mtu huyu hawi kafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 23/05/2019