Swali: Ipi hukumu ya yule mwenye kuwadharau watafutaji elimu na wanachuoni na anasema kuwa wana misimamo mikali na ni wasugu na kuwa hawajui mambo ya kisasa?

Jibu: Wakidharauliwa wanachuoni kwa dhati yao, hii ni dhambi ya wazi. Lakini akiwadharau na akakusudia kwa dharau hii kudharau Qur-aan na Sunnah, hii ni kufuru. Hali kama mlivyosikia. Tunachowanasihi ndugu zetu wawe na subira, wawe watulivu na wasome. Watu hawa wafanyoa kejeli ipo siku – In Shaa Allaah, watakuja kupata malipo yao yote:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

”Enyi mlioamini! Subirini na shindaneni kusubiri na kuweni macho na mcheni Allaah ili mpate kufanikiwa.” (3:200)

Hali kadhalika alisema Nuuh (´alayhis-Salaam) wakati watu walimdharau alipokuwa anatengeneza safina; akawaambia:

إِن تَسْخَرُواْ مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ

”Ikiwa nyinyi mnatukejeli [basi mjue na] sisi tunakukejelini kama mnavyo tukejeli.” (11:38)

Ninawanasihi kusubiri:

وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ

”Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.” (41:34)

Subirini Allaah Awabariki! Na Anasema Allaah (Subhaanah):

وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ

”Na Tukawafanya miongoni mwao waongozi wanaoongoa watu kwa amri Yetu, walipo subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu.” (32:24)

Na ninawanasihi kejeli hizi ziwafanye mpate moyo wa kushikamana bara bara na Sunnah na kujitahidi kutafuta elimu. Lau tungeliwatii hawa wanaotudharau, tungeliacha elimu na tungeacha Da´wah ya Allaah. Alikejeliwa yule ambaye ni mbora kuliko sisi. Alikejeliwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Mitume kabla yake. Ni juu yetu kusubiri, hii ni neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) juu yako ikiwa utakejeliwa [utapondwa] kwa ajili ya Da´wah. Wewe uko katika nafasi kubwa. Aliambiwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni mwendawazimu na kuwa ni mchawi: Msijali:

وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ

”Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.” (54:26)

وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ

”Na wanaodhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” (26:227)

Himidi zote ni Zake Allaah kwa kuwa watu wanazidisha chuku wanapoona Ahl-us-Sunnah wanakejeliwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/sounds.php?sound_id=33 Tarehe: 1420-12-18/2000-03-23
  • Imechapishwa: 09/04/2022