Swali: Mimi nina ndugu watatu na mimi ndiye mkubwa wao. Wako na wake na huwaamsha kuswali Subh kwa nguvu. Je, niwaache na dhambi zitakuwa juu ya waume zao au niwaamshe? Pamoja na kuzingatia kwamba wanawake hawa wanaswali lakini swalah Subh kwao ni ngumu.

Jibu: Maadamu mko katika nyumba moja na wewe ndiye mkubwa uliye nyumbani, basi lililo la wajibu kwako ni kuwaamrisha swalah wote waliyomo ndani ya nyumba na kuwatilia mkazo juu ya hilo. Ni mamoja ni waume, wanawake au watoto. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nyote ni wachungi na nyote mtaulizwa juu ya kile mlichokichunga.”

Lakini hata hivyo unatakiwa uwazungumzishe wanawake hawa na wewe ukiwa nje ya chumba ambacho hulala humo pindi unapotak kuwaamsha ili usije kuona sehemu zao za siri. Vivyo hivyo unapasa kuwanasihi wao na wake zao katihali hali ya wakiwa macho na mnapokusanyika. Labda hilo linawanufaisha na kuwahimiza kuamka kuswali Fajr ndani ya wakati wake pindi utawapozindua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/308)
  • Imechapishwa: 17/09/2021