Kuwa na ushabiki kwa Shaykh, kundi au madhehebu fulani ni katika mambo ya Jaahiliyyah

Moja katika yale madhehebu yanaweza kuwa bora kuliko mengine katika masuala fulani kwa kuafikiana kwake na Qur-aan na Sunnah. Wakati mwingine madheebu hayohayo yanaweza kushindwa kwa sababu ileile ya kuafikiana na Qur-aan na Sunnah. Kinazingatiwa ni kule kuafikiana na Wahy. Ama kufuata madhehebu maalum, kufanya ushabiki juu yake, kulingania kwayo, kuwa tayari kuridhika na kukasirika kwayo, haya ni miongoni mwa mambo ya kipindi cha makafiri. Vivyo hivyo inahusiana na mapote na makundi na mtu akawa na ushabiki juu ya pote fulani. Kama mfano wa pote la Suufiyyah au mrengo mwingine kama mfano wa falsafa au kundi miongoni mwa makungi mengine. Mtu akafanya kupenda na kuridhia ni kwa ajili yake na kuyafadhilisha juu ya mengine. Sambamba na hilo akawa anayaponda mengine. Yote haya ni miongoni mwa mambo ya kipindi cha kikafiri.

Kadhalika inahusiana na Mashaykh ambapo mtu akawa anamfuata Shaykh fulani na anaona kuwa yale yanayosemwa na Shaykh huyo tu ndio haki na yanayosemwa na Mashaykh wengine si lolote si chochote kwa njia ya kwamba kukatofautishwa kati ya Mashaykh na wanafunzi. Kuwa na ushabiki kwa Shaykh maalum ni miongoni mwa mambo ya kipindi cha kikafiri. Ni wajibu kuwaweka Mashaykh katika ngazi moja. Hakuna fadhilah kwa Shaykh juu ya mwingine isipokuwa kwa mujibu wa kule kuafikiana na Qur-aan na Sunnah, kuitendea kazi Qur-aan na Sunnah na kulingania katika Qur-aan na Sunnah. Wakati huohuo ikiwa Shaykh yuko na sifa hizi basi ana haki ya kumpenda na kusoma kwake. Lakini hata hivyo haijuzu kwake kufanya ushabiki naye kwa njia ya kwamba akaamini kuwa maneno yake tu ndio hoja. Hakuna yeyote, pasi na kuzingatia ile elimu, kumcha Allaah, matendo, wema, atayofikia, ambaye maneno yake yatakuwa ni hoja na dalili isipokuwa tu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hizi ni miongoni mwa khasara za kuwa na ushabiki kwa Mashaykh, madhehebu, makundi na mapote. Haya ni maneno ya Ibn-ul-Qayyim.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=163317
  • Imechapishwa: 01/09/2018