Kuwa na ami anayezungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud

Swali:  Nina ami ambaye anajinasibisha na kundi katika Mu´tazilah na anazungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud. Nimemnasihi mimi na wengine mara nyingi. Je, nimkate kwa ajili ya Allaah pamoja na kuendelea kumnasihi? Mimi nachelea juu ya watoto wangu akaingiza fikira zake kati yao. Nifanye nini na yeye?

Jibu: Kuzungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud ni kubaya zaidi kuliko kupinda kwake kwa Mu´tazilah au akawa ni mwenye kuzungumza kwa maoni ya Mu´tazilah. Mu´tazilah ni afadhali kidogo kuliko msemo wa Wahdat-ul-Wujuud. Wahdat-ul-Wujuud ni kufuru ya wazi kabisa. Wahdat-ul-Wujuud ni kufuru ya wazi kabisa ambayo ni mbaya zaidi kuliko kufuru ya Fir´awn. Maadamu hali yako iko namna hivyo na wewe una uhakika ya kwamba ana fikira na madhehebu hayo, jitenga naye mbali na uwatenge wana wako. Ukithibitisha kwake ya kwamba anasema maneno haya, haijuzu kumwacha. Ni lazima asimamishiwe hukumu ya Kishari´ah akiwa katika nchi ambayo kunasimamishwa hukumu ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (32) http://alfawzan.af.org.sa/node/2144
  • Imechapishwa: 13/07/2020