Kuvunja nia ya hajj peke yake na kwenda katika ´Umrah

Swali 13: Inajuzu kwa mtu ambaye amenuia Hajj peke yake kuivunja nia yake na kwenda katika ´Umrah? Bi maana baada ya kupita miyqaat?

Jibu: Ndio. Akihirimia Hajj imesuniwa kwake kuifanya ´Umrah ikiwa hakufikiria kuchinja. Ama ikiwa amenuia kuchinja ngamia, ng´ombe au kondoo, basi aendelee na ´ibaadah yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 28/09/2018